Chagua Maisha lived experiences: Changing lives for the better

Annabelle’s Story
Siku ya kwanza wakati wa mafunzo nilishuhudia ugumu wakati ambapo nilikua nauliza swali ama mchango kutoka kwa wasichana kumi niliokua nafunza lakini hawakunipa majibu ila tu kuniangalia. Baada ya kukutana na wao mara tatu, uhusiano wetu uliimarika, walianza kujibu maswali na kutoa maoni yao kwa ujasiri. Nilifurahi sana kufahamu kwamba mmoja wao aliamua kubadili mwelekeo wake kitabia nakuanza kutii wazazi wake. Alikua halali nyumbani bali kwa vijana wa mtaa jambo ambalo liliwakera wazazi wake.
Wasichana kumi hao, walishukuru sana kwa mafunzo waliopata kupitia Chagua Maisha curriculum. Walisema wanamudu wakati wao vyema na hata kutumia pesa vizuri baada ya kujifunza “Time management na Financial management”. Kati yao kulikua na aliyekua haendi shule kwa sababu zake mwenyewe licha ya karo kua. Aliamua kuwaomba msamaha wazazi wake kwa makosa aliyofanya na kwa sasa amerejea shule gredi ya nane na anasoma vyema. Himizo ya hali ilikua mafunzo kutoka kwa kufanya maamuzi mema “Making Good Choices”.
Nasema ahsante sana kwa ACLAD kwa mafunzo haya ya Chagua Maisha. Nimenufaika kiakili na hata kiujuzi. Nitaendelea kufunza wasichana wenzangu katika jamii.

Lucy’s Story
Nilishirikiana na Annabelle kuwafunza wasichana kumi Chagua Maisha curriculum huku Shitoli. Na kwa sababu Annabelle husoma katika chuo cha mabweni, nami shule ya kutwa, ilibidi mimi niendelee kuwafunza hao wasichana kumi hadi tukakamilisha mafunzo yote. Wanakijiji na hata wazazi waliwahimiza wasichana hawa kufuata mfano wangu na Annabelle ili wawe vielezo bora katika jamii.
Wengi wao walitembea ama kushirikiana na makundi mabovu lakini waliamua kubadilika mienendo hayo baada ya mafunzo ya Chagua Maisha. Mimi binafsi, Chagua Maisha imeniwezesha kupata ujasiri wa kusimama mbele ya umati na kuweza kuongea bila ya kuogopa. Naweza fanya maamuzi mema, kutumia wakati wangu vizuri na hata kujua marafiki wema ambao naweza kushirikiana nao kwa mambo ya masomo.
Asante sana ACLAD kwa huu mradi wa mafunzo kwa vijana.